Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 14:50:13    
New York-Jumuia ya kimataifa yazitaka Palestina na Israel kufikia makubaliano ya amani

cri
Mkutano wa kimataifa wa kuunga mkono watu wa Palestina tarehe 24 ulifanyika huko New York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kwenye mkutano huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alisema, Palestina na Israel zinapaswa kufikia makubaliano ya amani ili kujenga nchi ya Palestina inayoweza kuishi pamoja kwa amani na Israel na kutatua masuala mbalimbali yanayokumba nchi hizo mbili kwa muda mrefu.

Ban Ki-moon aliitaka Israel iache kujenga makazi ya kudumu na vitendo vingine vya upande mmoja vinavyobadili hali ya hivi sasa, na kupunguza vizuizi dhidi ya Gaza. Na alitoa mwito pia ya kuyataka makundi yote ya Palestina yafanye jitihada za kutimiza umoja wa ukanda wa Gaza na kando za magharibi wa Mto Jordan.