Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 15:15:28    
Bissau-Bw. Javier Solana Madariaga afuatilia hali ya Guinea-Bissau

cri

Mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Ulaya anyeshughulikia mambo ya kidiplomasia na sera za usalama Bw. Javier Solana Madariaga tarehe 24 alitoa taarifa akifuatilia sana hali ya hivi sasa ya Guinea-Bissau.

Katika taarifa yake Bw. Solana alisema, anafuatilia sana tukio la ikulu ya Guinea-Bissau kushambuliwa kwa bunduki na baadhi ya wanajeshi wa nchi hiyo, na kutoa pole kwa watu waliokufa na kujeruhiwa katika shambulizi hilo. Bw. Solana alisema, matokeo ya uchaguzi mkuu wa Guinea-Bissau uliofanyika tarehe 16, mwezi huu yanapaswa kuheshimiwa. Bw. Solana alihimiza pande mbalimbali za kisiasa za Guinea-Bissau ziimarishe ushirikiano ili kuhakikisha mazingira ya utulivu yanayohitajika kwa maendeleo ya nchi hiyo.