Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 15:19:57    
Algiers-Algeria yataka kushirikiana na China katika kuwaandaa mafundi na wasimamizi wa miradi wa Algeria

cri

Waziri wa miradi ya umma wa Algeria Bw. Amar Ghoul tarehe 24 huko Algiers alisema, Algeria ina matumaini ya kuzidisha ushirikiano na China, Japan na Canada katika kuwaandaa mafundi na wasimamizi wa miradi ya uhandisi kuharakisha ujenzi wa miundombinu ya Algeria

Bw. Ghoul aliposhiriki kwenye sherehe ya kuanzisha semina ya pili ya wahandisi bora wa Algeria watakaosomea nchini China alisema, Algeria ina matumaini kuwa makampuni ya China, Japan na Canada yanapoanzisha miradi mikubwa ya umma, yatasaidia Algeria kuwaandaa mafundi na wasimamizi wa miradi.

Ofisa mhusika wa mradi wa barabara la mwendo kasi inayotoka mashariki hadi magharibi ya Algeria ambao unajengwa na kampuni ya China Bw. Hua Dongyi alisema, upande wa China umefanya maandalizi mazuri kwa kuwapokea wahandisi bora wa Algeria watakaokuja China kushiriki kwenye semina.