Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 18:39:35    
Chicago-Obama ateua rasmi wajumbe muhimu watakaoshughulikia mambo ya uchumi kwenye serikali mpya

cri
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Rais mteule wa Marekani Barack Obama tarehe 24 huko Chicago aliwateua rasmi wajumbe muhimu watakaoshughulikia uchumi kwenye serikali mpya, wakiwemo pamoja na waziri wa fedha, mkurugenzi wa kamati ya uchumi wa nchi na mkurugenzi wa kamati ya washauri wa uchumi ya Ikulu.

Bw. Obama alimteua rasmi mkuu wa benki ya akiba ya Marekani Bw. Timothy Geithner kuwa waziri wa fedha, na kumteua Bw. Lawrence Summers aliyekuwa waziri wa fedha wakati wa utawala wa Bill Clinton na mkuu wa Chuo Kikuu cha Harvard kuwa mkurugenzi wa kamati ya uchumi wa nchi, pia amemteua mtaalam wa uchumi wa Chuo Kikuu cha California Berkeley Bi. Christina Romer kuwa mkurugenzi wa kamati ya washauri wa uchumi ya Ikulu.