Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 19:34:52    
Athari ya msukosuko wa fedha duniani kwa uchumi wa China yaweza kudhibitiwa kwa hivi sasa

cri

Ripoti iliyotolewa tarehe 25 hapa Beijing na Benki ya Dunia kuhusu uchumi wa China inasema, hivi sasa athari iliyosababishwa na msukosuko wa fedha na uchumi duniani kwa uchumi wa China iko katika hali ya kuweza kudhibitiwa, lakini athari hiyo itaongezeka.

Mtaalamu mwandamizi wa benki hiyo Bw. Louis Kuijs alisema, mfumo wa fedha wa China unatengana na soko la fedha la kimataifa, hivyo unaweza kuepuka na athari ya moja kwa moja iliyosababishwa na msukosuko wa fedha. Kwa upande mwingine, mauzo ya bidhaa za China katika nchi za nje bado yanaongezeka kwa kasi, lakini mwaka kesho ongezeko hilo litapungua.

Ripoti hiyo pia inakadiri kuwa mwaka 2009 ongezeko la thamani ya uzalishaji mali nchini China litakuwa karibu asilimia 7.5.