Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 19:45:42    
Nairobi-Afrika Mashariki yaunda jeshi ili kupambana na maharamia

cri
Gazeti la Daily Nation la Kenya tarehe 25 lilitoa habari kuwa, nchi za Afrika Mashariki hivi karibuni limeunda jeshi lenye watu 7000 nchini Kenya ili kukabiliana na msukosuko wa usalama ulioibuka ghafla katika sehemu hiyo, lengo hasa la jeshi hilo ni kupambana na vitendo vya maharamia vinavyotokea mara kwa mara katika sehemu ya pwani ya Somalia.

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bw. Moses Wetangula tarehe 24 alisema, jeshi hilo la Afrika Mashariki litatekeleza jukumu la kukabiliana na msukosuko wa usalama ulioibuka ghafla katika sehemu hiyo, na pia limefanya maandalizi mazuri ya kwenda kwenye sehemu ya pwani ya Somalia kupamabana na maharamia.

Bw. Wetangula aliongeza kuwa, kazi muhimu za jeshi hilo si kulinda amani tu, bali pia linapaswa kufuatilia dalili yoyote inayotishi usalama, na mara tu baada ya kugundua dalili ya hali yoyote isiyo ya usalama kwenye sehemu hiyo, jeshi hilo linatakiwa kuchukua hatua ili kudhibiti hali ya mambo.