Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 19:46:43    
Jerusalem-Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao apongeza mkutano wa "Siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina"

cri

Mkutano wa maadhimisho ya "Siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina" tarehe 24 ulifanyika huko New York, makao makuu ya Umoja wa Mataifa, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alitoa salamu za pongezi kwa mkutano huo.

Katika salamu hizo Bw. Wen Jiabao amesema, suala la Palestina ni kiini cha suala la mashariki ya kati, China inawaunga mkono kithabiti wananchi wa Palestina warudishe haki halali ya kitaifa, na kuunga mkono mchakato wa amani wa mashariki ya kati. China inazitaka Palestina na Israel zishikilie njia ya mazungumzo ya amani na nchi huru ya Palestina ianzishwe mapema iwezekanavyo chini ya msingi wa maazimio husika ya Umoja wa Mataifa na kanuni ya "kubadilishana amani kwa ardhi" ili kutimiza lengo la kuishi pamoja kwa amani kwa nchi mbili za Palestina na Israel.

Aidha Bw. Wen amesema, China ikiwa ni mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama itaendelea kuunga mkono Umoja wa Mataifa uoneshe umujimu wake katika suala la mashariki ya kati, na China itafanya juhudi pamoja na jumuia ya kimataifa kusukuma mbele utatuzi wa suala la Palestina, na kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya sehemu ya mashariki ya kati.