Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-25 21:15:34    
Athens-Rais wa China akutana na viongozi wa vyama vya Ugiriki

cri

Rais Hu Jintao wa China ambaye yuko ziarani nchini Ugiriki tarehe 25 huko Athens kwa nyakati tofauti amekutana na mwenyekiti wa Chama cha Kisoshalisti cha Ugiriki Bw. George Papandreou na katibu mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo bibi Aleka Papariga.

Alipokutana na Bw. Papandreou rais Hu amesema uhusiano kati ya Chama cha Kikomunisti cha China na Chama cha Kisoshalisti cha Ugiriki umekuwa sehemu muhimu katika uhusiano wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili, na Chama cha Kikomunisti cha China kinapenda kuongeza mawasiliano na ushirikiano kati yake na Chama cha Kisoshalisti cha Ugiriki, ili kuhimiza uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya China na Ugiriki uendelezwe siku hadi siku.

Alipokutana na bibi Papandreou, rais Hu amesema Chama cha Kikomunisti cha China kinapenda kuimarisha uhusiano kati yake na Chama cha Kikomunisti cha Ugiriki kwa kufuata kanuni za uhuru na kujiamulia, usawa kamili, kuheshimiana na kutoingilia mambo ya ndani.