Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-26 19:04:38    
China yapata mafanikio katika kuzuia magendo makubwa

cri

Habari zilizotolewa tarehe 26 na idara kuu ya forodha ya China zinasema, tangu kikosi cha polisi wa forodha wa kupambana na uhalifu wa magendo kianzishwe miaka 10 iliyopita, kimeshughulikia kesi zaidi ya 12,000 za uhalifu wa magendo ya aina mbalimbali ambayo yana thamani ya yuan zaidi ya bilioni 150, kuadhibu watuhumiwa zaidi ya elfu 30 wa magendo, na kufanikiwa kuzuia mwelekeo wa kufanya shughuli kubwa za magendo makubwa.

Hali kadhalika kikosi hicho cha China pia kilishirikiana na nchi na sehemu mbalimbali katika kupambana na uhalifu wa dawa za kulevya.