Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-26 19:40:32    
China yatenga yuan zaidi ya bilioni 30 katika mambo yanayohusu kilimo, vijiji na wakulima

cri

Mkurugenzi wa idara ya uchumi wa vijiji ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Gao Juncai tarehe 26 amesema, kati ya nyongeza za uwekezaji zilizotolewa na serikali kuu kwenye robo ya nne ya mwaka huu, yuan zaidi ya bilioni 30 zitatumiwa katika mambo yanayohusu kilimo, vijiji na wakulima.

Bw. Gao Juncai amesema pesa hizo zitatumiwa katika miradi ya kuhakikisha usalama wa maji ya kunywa, chakula, kukinga mafuriko ya maji, uhifadhi wa mazingira, sifa za mazao ya kilimo, maliasili ya maji na nyinginezo.