Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-26 19:43:14    
Prague-Ireland kurudia tena upigaji kura za maoni ya raia wote kuhusu mkataba wa Lisbon

cri

Waziri wa Ireland anayeshughulikia mambo ya Ulaya Bw. Dick Toche tarehe 25 huko Prague alisema, raia wote wa Ireland watapiga kura tena za maoni kuhusu mkataba wa Lisbon.

Bw. Roche alisema, upigaji kura mpya za maoni ya raia wote utafanyika baada ya kuwasiliana na Umoja wa Ulaya kwa uvumilivu na kuondoa wasiwasi wa raia wa Ireland kuhusu mkataba wa Lisbon.

Alisema, Ireland inasisitiza kuwa lazima awepo mjumbe mmoja wa kila nchi katika kamati ya Umoja wa Ulaya, na kuutaka Umoja wa Ulaya uwe na haki ya kupiga kura ya veto juu ya masuala ya uhuru wa jeshi, kupinga uhalibu wa mamba na kiwango cha ushuru cha pamoja. Ireland inaona kuwa ni mamlaka ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuamua ushuru wake wa nchi.