Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-26 20:01:34    
New York -Mjumbe wa China asisitiza ni lazima suala la Mashariki ya Kati litatuliwe kwa njia ya mazungumzo ya kisiasa

cri

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Yesui tarehe 25 alipotoa hotuba kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa alisema, mazungumzo ya kisiasa ni njia pekee ya kutatua suala la Mashariki ya Kati.

Baraza kuu la 63 la Umoja wa Mataifa siku hiyo liliitisha mkutano kujadili suala la Palestina na hali ya Mashariki ya Kati. Bw. Zhang Yesui alisisitiza kuwa, mazungumzo ya kisiasa ni njia pekee ya kutatua suala la Mashariki ya Kati. Katika hali ya hivi sasa, Palestina na Israel zinapaswa kushikilia kithabiti imani ya kuendeleza mchakato wa mazungumzo ya amani katika hali yoyote. China inazitaka Palestina na Israel zishikilie utaratibu wa mazungumzo katika hali mpya ili mazungumzo hayo yaweze kupata maendeleo mapya, nchi huru ya Palestina ianzishwe mapema iwezekanavyo na nchi mbili za Palestina na Israel ziweze kuishi pamoja kwa amani kwa kufuata maazimio husika ya Umoja wa Mataifa na kanuni ya "kubadilishana amani kwa ardhi".

Aidha, China inatoa mwito wa kuitaka jumuiya ya kimataifa iendelee kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa Palestina.