Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-26 21:02:10    
Teknolojia za juu zarahisisha maisha ya watu

cri
Bidhaa nyingi za teknolojia za kisasa kama hizo hivi karibuni zilioneshwa kwenye maonesho ya 10 ya teknolojia mpya na za hali ya juu ya kimataifa ya China yaliyofanyika huko Shenzhen.

Kwenye jumba la maonesho hayo, bandi moja ya muziki wa jadi inayoundwa na watu 10 ilikuwa inapiga muziki. Lakini tofauti na hali ya kawaida, kuna skrini mbele ya kila mpiga mziki badala ya karatasi za muziki kama kawaida. Profesa wa chuo cha muziki cha China Bw. Fan Zuyin alisema, karatasi za muziki ni chombo kisichokosekana kwa wapiga mziki wa ala, lakini wanabidi kufungua ukurasa kila baada ya muda. skrini hiyo imeondoa tatizo hilo, kwa kuwa inaweza kufungua ukurasa mwenyewe kwa kwenda sambamba na muziki zinazopigwa. Bw. Fan Zuyin alisema:

"pia kuna watu wengine duniani wanaoendelea kufanya utafiti kuhusu teknolojia hii, lakini bado hawajafanikiwa. Hivi sasa nchini China teknolojia hiyo imeanza kutumikwa kwenye bandi maalumu, kwa upande huo, China imetangulia duniani."

Mbali na skrini hiyo, pia kuna bidhaa nyingi nyingine za teknolojia ya juu zinazorahisisha maisha ya watu zilitolewa kwenye maonesho hayo. Maonesho hayo yaliyoanza kufanyika mwaka 1999 kila mwaka yanasifiwa kuwa ni maonesho ya kwanza ya sayansi na teknolojia nchini China, kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu ni "sayansi na teknolojia huboresha maisha ya watu, uvumbuzi hubadilisha dunia". Kwa mfano, makampuni ya televisheni ya China yalionesha bidhaa zao mpya, uunganisho wa usanifu maalumu na teknolojia mbalimbali umeifanya televisheni iwe na uwezo mbalimbali mpya.

Kwenye kibanda cha maonesho cha kampuni ya Konka, televisheni moja maalumu iliwavutia watazamaji wengi. Mtazamaji mmoja aliyevaa glavu maalumu alipotikisa mkono, televisheni ilibadilisha idhaa, na alipogeuza mkono, televisheni ilipunguza au kuongeza sauti.

Bw. Wang wa kampuni ya Konka alieleza kuwa sirisiri ya televisheni hiyo ni glavu yake. Glavu hiyo yenye uwezo wa kuakisi mionzi ya ultrared ray inaweza kutafsiri vitendo vya mkono na kudhibiti televisheni. Bw. Wang alisema,

"nadhani vijana watapenda televisheni ya aina hiyo. michezo mingi ya hivi sasa inasaidia kujenga afya, tunapanga kutengeneza aina mpya za televisheni zenye umaalum wa kibinafsi na mtindo wa kisasa, na zinazingatia zaidi mahitaji ya watu wa ngazi tofauti na wa makundi tofauti."

Baadhi ya watazamaji walipohojiwa walisema, maendeleo ya sayansi na teknolojia yameleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya binadamu, hata mambo ambayo hayakufikiriwa zamni hivi sasa yamekuwa wa kweli.

Kwenye maonesho hayo, pia kulikuwa na maonesho ya maeneo maalumu ikiwemo teknolojia za juu za ndege na za safari za anga ya juu. Mwezi Septemba, mradi wa chombo cha safari ya anga ya juu kinachobeba wanaanga cha Shenzhou No. 7 ulimalizika kwa mafanikio, na katika safari hiyo watu wa China kwa mara ya kwanza walitembea nje ya chombo kwenye anga ya juu. Baadhi ya vitu vilivyoko kwenye chombo hicho pia vilioneshwa kwenye maonesho hayo, kama vile saa wanaanga walizozivaa na vitanda vilivyoko chombo hicho. Aidha wanasayansi wa China pia walionesha maendeleo na matokeo ya utafiti wa roboti ya anga. Mwanachama wa taasisi ya uhandisi ya China Bw. Cai Hegao alisema, China itarusha saitelaiti moja mwaka 2011 na kuanza kufanya majaribio ya mkono wa "roboti ya anga" .

Mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 17 ya chama cha kikomunisti cha China uliofungwa mwezi Oktoba uliweka mpango mpya wa kimkakati kuhusu mageuzi na maendeleo ya sehemu za vijiji nchini China. kwa hiyo namna ya kutumia teknolojia za juu katika kusukuma mbele maendeleo ya kilimo ni suala jingine lililofuatiliwa sana kwenye maonesho hayo. Kama tunavyojua, China imefanikiwa kulisha asilimia 22 ya idadi ya watu duniani kwa kutumia asilimia 7 ya eneo la shamba duniani. Teknolojia za kisasa za kilimo zilitoa mchango mkubwa katika kuinua uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuhakikisha usalama wa chakula nchini China.

Kutoka michele na mipunga iliyooteshwa kwa teknolojia ya juu hadi teknolojia ya kisasa ya mwagiliaji, maonesho hayo yalionesha kwa jumla matokeo ya miradi ya teknolojia ya kilimo kutoka sehemu mbalimbali nchini China. kwenye kibanda kimoja mwandishi wetu wa habari aliona maonesho ya teknolojia mpya ya kupanda minazi. Mfanyabiashara Bw. Gan Donghai alisema, zamani wakulima wa mkoa wa Hainan walipanda minazi kwenye shamba dogo mbele ya nyumba yao tu na kuuza nazi zilizovunwa. Lakini sasa kwa kutumia teknolojia hiyo, mkoa wa Hainan umekuwa na shamba la minazi lenye eneo kubwa.

Imefahamika kuwa, hivi sasa teknolojia hiyo mpya imeenezwa kwenye mikoa majirani ya Guangdong na Guangxi, nazi imekuwa moja ya mazao ya kibiashara yanayoongeza pato la wakulima wa sehemu hizo.

Kutoka teknolojia za juu za ndege na za safari za anga ya juu hadi uvumbuzi wa teknolojia za vyombo vya umeme nyumbani, kutoka bidhaa za kielektroniki hadi mibegu bora ya mazao ya kilimo, teknolojia zilizooneshwa kwenye maonesho hayo nusura zinahusisha kila upande wa maisha ya watu, na yameunganisha zaidi sayansi na teknolojia mpya na maisha ya kila siku.