Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-26 21:05:25    
Mwezi Oktoba kiwango cha matarajio ya uchumi wa China chaendelea kushuka lakini bado kiko kwenye hali ya utulivu

cri

Idara ya takwimu ya China tarehe 26 imetangaza matokeo ya uchunguzi wake kuwa, mwezi Oktoba kiwango cha matarajio ya uchumi wa China kilikuwa 94.7, kimepungua kwa 10.6, lakini bado kiko kwenye kiwango cha utulivu.

Kiwango cha matarajio ya uchumi kama kikifikia 100, hiki kitakuwa kiwango kinachotarajiwa. Uchunguzi umeonesha kuwa, kuanzia mwezi Juni mwaka huu, kiwango hicho kimeanza kushuka kwa miezi mfululizo kutoka 112 mwezi Juni, hadi 105.3 mwezi Agosti, na mpaka 94.7 mwezi Oktoba.