Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-27 14:54:13    
New York- Baraza la Usalama lasikiliza ripoti kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 26 lilisikiliza ripoti kuhusu hali mpya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ripoti hiyo ilishauri kuanzisha utaratibu wenye ufanisi wa kukabiliana na mgogoro wa kimabavu utakaotokea kwenye sehemu hiyo, ili kuhakikisha mazungumzo ya amani yanaendelea vizuri.

Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bw. Alan Doss alilifahamisha Baraza la Usalama ripoti iliyotolewa hivi karibuni na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon, akisema mgogoro uliotokea hivi sasa huko jimbo la Kivu Kaskazini umeingia kwenye kipindi chenye hatari na umeathiri uokoaji wa kibinadamu na raia wengi kujeruhiwa.

Ripoti hiyo pia lilisisitiza Baraza la Usalama lirefushe muda wa tume maalumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mwaka mmoja yaani kufikia mwishoni mwa mwaka 2009, pia inalitaka Baraza la Usalama lijadili uundaji wa tume maalumu na jukumu lake katika kipindi chake cha mwaka kesho.