Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-27 15:44:42    
China kuisaidia Zimbabwe kwa chanjo ya kipindupindu

cri
Balozi mdogo wa China nchini Zimbabwe He Meng tarehe 26 alisema China itaisaidia Zimbabwe kwa chanjo za kipindupindu kutokana na nchi hiyo kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo.

Bw. He Meng alisema China itatoa msaada wa chanjo za kipindupindu wenye thamani ya dola za Marekani laki tano kwa Zimbabwe haraka iwezekanavyo, mbali na msaada huo wa chanjo pia itatoa msaada wa chakula ili kupunguza hali mpya ya uhaba wa chakula nchini humo.