Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-27 18:30:26    
China kuwekeza yuan trilioni 5 katika ujenzi wa reli

cri

Naibu waziri wa reli wa China Bw. Lu Dongfu tarehe 27 hapa Beijing ametangaza kuwa, kuanzia sasa hadi mwaka 2020, China itajenga reli zenye urefu wa kilomita elfu 40, na uwekezaji wa jumla katika ujenzi wa reli utazidi yuan trilioni 5.

Bw. Lu Dongfu amesema miradi ya reli inayopangwa ni mahitaji ya maendeleo ya uchumi na jamii, uzalishaji na maisha ya raia. Miradi hiyo ni pamoja na reli ya abiria, reli kati ya miji, reli ya uchukuzi wa makaa, na reli muhimu za magharibi mwa China. Amesema ujenzi wa reli yenye urefu mkubwa namna hii na kuwekezwa mtaji mkubwa haujawahi kutokea katika historia ya ujenzi wa reli nchini China. Bw. Lu Dongfu amedokeza kuwa hadi kufikia mwaka 2020 reli nchini China zitafikia urefu wa kilomita zaidi ya laki 1.2.