Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-27 19:10:02    
Kiwango cha madeni ya fedha yanayobebwa na serikali ya China kiko kwenye hali ya usalama na ya kufaa

cri
Mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Zhang Ping tarehe 27 amesema hapa Beijing kuwa, hivi sasa kiwango cha madeni ya fedha yanayobebwa na serikali ya China bado kiko kwenye hali ya usalama na ya kufaa.

Bw. Zhang aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku hiyo alipojibu swali la mwandishi wa habari kuhusu "serikali ya China imepanga mpango wa kuongeza uwekezaji mwingine wa trilioni 4, je, mpango huo utaweza kuzifanya serikali za mitaa zibebe madeni zaidi ya kupita kiasi au la?"

Bw. Zhang amesema, katika mpango wa uwekezaji wa hatua ijayo, kweli serikali za mitaa zinatakiwa kutenga fedha kwa kiasi fulani. Hivi sasa idara husika za China zinajadili namna ya kupunguza mzigo wa fedha wa serikali za mitaa.