Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-27 19:38:01    
Rais Hu Jintao wa China amaliza ziara yake barani Latin Amerika na Ulaya

cri

Tarehe 27 rais Hu Jintao wa China amerudi Beijing baada ya kumaliza ziara yake barani Latin Amerika na Ulaya.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Yang Jiechi ambaye aliambatana na rais Hu Jintao aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ziara hiyo imetimiza lengo la kuimarisha urafiki na uaminifu, kupanua ushirikiano, na kutafuta maendeleo ya pamoja kwa ujumla, imepata mafanikio makubwa.

Bw. Yang Jiechi alisema, hali ya fedha duniani inazidi kuwa mbaya siku hadi siku, uhusiano kati ya China na Amerika ya Kusini na Ugiriki umeingia katika kipindi kipya cha maendeleo?kutokana na hali hiyo ziara hiyo ya rais Hu Jintao ina umuhimu mkubwa wa kuimarisha ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa, kuukabili kwa pamoja msukosuko wa fedha, na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na Latin Amerika na Ugiriki.