Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-27 19:42:18    
China yapenda kufanya juhudi pamoja na Ulaya ili kulinda na kusukuma mbele maendeleo mazuri ya utulivu ya uhusiano kati yao

cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Qin Gang tarehe 27 kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hapa Beijing alisema, China inapenda kufanya juhudi pamoja na Ulaya ili kulinda na kusukuma mbele maendeleo mazuri ya utulivu ya uhusiano kati yao.

Bw. Qin Gang siku hiyo alipojibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu China kuahirisha mkutano wa 11 wa viongozi wa China na Ulaya alisema, ufunguzi wa mkutano wa 11 wa viongozi wa China na Ulaya unategemea lini nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya, Ufaransa itachukua hatua halisi za kujenga mazingira ya lazima yenye hali nzuri kwa mkutano huo. Bw. Qin Gang alisema, kuzidisha na kukuza uhusiano kati ya China na Ulaya kunanufaisha pande zote mbili na dunia nzima, hasa katika hali ya hivi sasa China na Umoja wa Ulaya zinatakiwa kuzidisha ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za dunia zikiwemo msukosuko wa fedha wa duniani, usalama wa chakula na nishati na mabadiliko ya hali ya hewa.