Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-28 09:59:00    
Vienna- Mjumbe wa China aeleza msimamo wa China kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea na suala la nyuklia la Iran

cri

Mjumbe wa ofisi ya kudumu ya China huko Vienna ambaye pia ni mjumbe wa China kwenye jumuiya nyingine Bw. Tang Guoqiang tarehe 27 katika mkutano wa baraza la Shirika la Nishati ya Atomiki ya Dunia alitoa hotuba akieleza msimamo wa China kuhusu suala la nyuklia ya Peninsula ya Korea na suala la nyuklia ya Iran.

Bw. Tang alisema, suala la nyuklia ya Peninsula ya Korea linahusika na amani na utulivu wa sehemu hiyo na Kaskazini mashariki ya Asia, China inaunga mkono kutatua suala hilo kwa njia ya amani, yaani kufanya mazungumzo, pia inaunga mkono kutimiza lengo la kuifanya peninsula hiyo iwe sehemu isiyo na nyuklia, kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo na sehemu ya Asia ya kaskazini na mashariki.

Bw. Tang alipoeleza suala la nyuklia ya Iran alisema, China siku zote inaunga mkono na kulinda mfumo wa kimataifa wa kutoeneza silaha za nyuklia, inaunga mkono kutatua suala la nyuklia ya Iran kwa njia ya amani, ili kulinda amani na utulivu wa sehemu ya Mashariki ya Kati.