Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-28 16:27:34    
China kuimarisha zaidi ushirikiano wa kimataifa wa kilimo

cri

Naibu waziri wa kilimo wa China Bw. Niu Dun tarehe 27 huko Nanning, mkoani Guangxi, China alisema, kutokana na kukabiliwa na hali mpya duniani yenye utatanishi, idara za kilimo zitaimarisha zaidi ushirikiano wa kimataifa wa kilimo.

Kwenye mkutano wa kazi ya China ya ushirikiano wa kimataifa wa kilimo, Bw. Niu Dun alisema sasa ushirikiano wa kimataifa wa kilimo unakabiliwa na mazingira yenye utatanishi na mabadiliko mengi duniani, na idara za kilimo nchini China zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kwenye sekta ya nafaka, na kuhimiza biashara ya mazao ya kilimo iendelezwe kwa utulivu, vilevile zinapaswa kuimarisha ushirikiano wa kilimo na nchi za nje, na kuimarisha kazi ya kuwaandaa watu wenye ujuzi kuhusu ushirikiano wa kimataifa wa kilimo.