Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-28 18:32:54    
Vienna-Mkutano wa baraza la Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki wafanyika huko Vienna

cri
Mkutano wa baraza la Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA ulifanyika tarehe 27 katika makao makuu ya shirika la IAEA huko Vienna. Suala la Syria ni mojawapo ya masuala muhimu yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wanadiplomasia kwenye shirika hilo walikadiria kuwa uko uwezekano ambao Marekani itafanya juhudi za kufikia makubaliano kuhusu suala la Syria kwenye mkutano huo ili kuiwekea Syria shinikizo zaidi, lakini hakuna uwezekano mkubwa kupata uungaji mkono wa nchi nyingi wanachama.

Kwenye mkutano huo, mkurugenzi mkuu wa shirika la IAEA Bw. Mohamed M. El Baradei alizikosoa Marekani na Israel kufanya ukaguzi kuhusu suala la Syria. Alisema, Marekani na Israel zilichukua hatua zenye nguvu za upande mmoja kwa majengo yanayoitwa mashaka ya Syria na baadaye zilitoa habari kuhusu kuharibiwa kwa majengo hayo. Vitendo hivyo vimezuia vibaya shirika la IAEA kuchambua na kutoa maamuzi.