Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-28 18:42:11    
China yataka kudumisha mazungumzo kiuchumi ya kimkakati kati yake na Marekani kuhusu uchumi wa kimkakati

cri

China na Marekani tarehe 4, mwezi Desemba hapa Beijing zitafanya mazungumzo ya tano kuhusu uchumi wa kimkakati, msaidizi wa waziri wa fedha Bw. Zhu Guangyao tarehe 27 alipokutana na waandishi wa habari wa China na Marekani alisema, China inataka kudumisha mazungumzo kati yake na Marekani kuhusu uchumi wa kimkakati.

Bw. Zhu alisema, utaratibu wa mazungumzo ya uchumi wa kimkakati kati ya China na Marekani umeonesha umuhimu wake mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara hata ushirikiano wa kiujenzi kati ya nchi hizi mbili.

Bw. Zhu aliongeza kuwa, katika mazingira magumu ya hivi sasa ya kukabiliwa na changamoto ya msukosuko wa fedha, China na Marekani zinatakiwa kuimarisha mawasiliano, kupashana habari na kuratibu sera za uchumi wa jumla. Hayo ni mambo muhimu sana katika kukabiliana na msukosuko wa fehda, kutuliza soko la fedha la kimataifa na kurudisha ongezeko la uchumi.