Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-29 18:27:39    
Lilongwe-Rais Mutharika wa Malawi apewa Tuzo ya Kilimo ya Shirika la FAO

cri
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Bw. Jacques Diouf tarehe 27 alimpa Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi Tuzo ya Kilimo ya Shirika la FAO, ili kusifu mchango aliotoa kwa maendeleo ya kilimo ya nchi hiyo katika miaka 4 iliyopita.

Tuzo la Kilimo ni tuzo ya ngazi ya juu kabisa katika Shirika la FAO, na hutolewa kwa nchi au watu waliotoa mchango mkubwa kwa kuondoa njaa na umaskini duniani. Rais Mutharika ni mtu wa 6 wa Afrika aliyepewa tuzo hiyo.

Katika miaka 3 iliyopita, serikali ya Malawi ilichukua sera mbalimbali za mageuzi ya kilimo na utoaji wa ruzuku. Rais Mutharika alisema, katika miaka ya hivi karibuni, uzalishaji wa nafaka nchini Malawi umeongezeka kwa kiasi kikubwa, licha ya kujitosheleza katika chakula, pia iliweza kuuza chakula kwa nchi za nje.