Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-11-30 19:03:41    
Doha- Rais wa Tanzania asisitiza kuwa Afrika inafuatilia hali ya utekelezaji wa Makubaliano ya Monterrey

cri

Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania tarehe 29 alisisitiza kuwa, Afrika inafuatilia sana hali ya jumuiya ya kimataifa kutekeleza Makubaliano ya Monterrey ambayo yalifikiwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2002 ili kuondoa umasikini na kuhimiza maendeleo.

Kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa ulioendelea baada ya mkutano wa ukusanyaji wa mitaji ya maendeleo ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa, kwa niaba ya upande wa Afrika Rais Kikwete alitoa hotuba akiitaka jumuiya ya kimataifa itoe misaada kwa pamoja kwa maendeleo ya uchumi ili kukabiliana na mkusosuko wa fedha duniani.

Rais Kikwete alisema, nchi za Afrika zimetekeleza majukumu yao, kuboresha mazingira ya uwekezaji, kufanya mageuzi ya kisiasa, kujenga mfumo wa sheria, kuboresha hali ya haki za binadamu, ambapo yamepata maendeleo makubwa katika sekta ya uendelezaji wa maliasili yenyewe, lakini maliasili hizo hazitoshelezi mahitaji ya maendeleo yao. Rais Kikwete aliitaka jumuiya ya kimataifa iongeze nguvu ya kutoa misaada ya kifedha kwa nchi za Afrika.