Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-01 14:47:18    
Khartoum-Holmes ataka kuharakisha mchakato wa kutatua kisiasa suala la Darfur

cri
Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia utoaji misaada ya kibinadamu Bw. John Holmes tarehe 30 mwezi huu huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan alitoa mwito na kutaka kuharakisha mchakato wa kutatua suala la Darfur kwa njia ya kisiasa.

Bw. Holmes siku hiyo alimaliza ziara yake ya siku 6 nchini Sudan. Kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, kadiri migogoro ya Darfur inavyodumu kwa muda mrefu, ndivyo mchakato wa kurudisha hali ya utulivu unavyozidi kuwa ngumu. Baada ya kuamua kusimamisha vita kwenye sehemu ya Darfur, serikali ya Sudan inapaswa kuharakisha mchakato wa kutatua suala la Darfur kwa njia ya kisiasa ili kutimiza utulivu na maendeleo ya sehemu hiyo.