Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-02 15:13:38    
Chicago-Rais mteule wa Marekani Barack Obama atangaza watu wake wa serikali mpya

cri
Rais mteule wa Marekani Barack Obama tarehe mosi Desemba huko Chicago kwenye mkutano na waandishi wa habari alitangaza watu wake wa serikali mpya.

Kwenye mkutano huo Rais mteule Barack Obama alimteua rasmi Bi Hillary Cliton, mbunge wa jimbo la New York kuwa waziri wa mambo ya nje na kumbakiza madarakani waziri wa ulinzi wa sasa Bw. Robert Gates. Bi. Hillary alisema atashirikiana barabara zaidi na jumuyia ya kimataifa katika kupambana na changamoto duniani na kujitahidi kuboresha sura ya Marekani duniani ili itoe mchango mkubwa zaidi.

Bw. Obama alisema, masuala ya Iran, Korea ya Kaskazini na mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati ni masuala yanayopewa kipaumbele kutatuliwa na serikali mpya katika mambo ya nje. Bw. Obama pia alisema Marekani inatakiwa kuendelea kuwa na nguvu kubwa zaidi ya kijeshi duniani. Alisema, Marekani inatakiwa kutumia nguvu za kijeshi, siasa na diplomasia kwa pamoja ili kuhuisha na kuimarisha uhusiano wake na nchi washirika, kuongeza maslahi ya Marekani, na kulinda usalama wake.

Bw. Obama alisisitiza kuwa atatekeleza ahadi yake ya kuondoa jeshi la Marekani kutoka Iraq ndani ya miezi 16 baada ya kushika madaraka ya urais, na kuhamisha nguvu za kupambana na ugaidi katika nchi ya Afghanistan.