Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-02 15:15:48    
New York-Kiongozi wa ujumbe wa Marekani wa mazungumzo ya Nyuklia aanza ziara yake ya nchi tatu za Asia

cri
Naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Robert Wood tarehe 1 alisema, kiongozi wa ujumbe wa Marekani kwenye mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea ambaye pia ni naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Christopher Hill siku hiyo alianza ziara yake nchini Japan, Singapore na China.

Siku hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Bw. Wood alisema, katika kipindi cha ziara hiyo Bw. Hill na Mkurugenzi wa idara ya mambo ya Korea Kusini katika Wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bw. Kim Sung watafanya mazungumzo na maofisa husika wa nchi hizo tatu, na kuhudhuria mkutano wa viongozi wa ujumbe wa mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea utakaofanyika tarehe 8 mjini Beijing, ambapo Bw. Hill pia atafanya mazungumzo na wajumbe wa pande nyingine tano kwa nyakati tofauti.