Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-02 15:17:10    
Geneva-Umoja wa Mataifa wadai kuacha ukiukaji wa haki za binadamu kwenye mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

cri
Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa tarehe 1 mwezi wa Desemba kwenye makao makuu yake, huko Geneva lilitoa mwito wa kuacha mara moja ukiukaji wa haki za binadamu katika sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na pia kuzitaka pande zote husika zitoe urahisi kwa kazi ya upelekaji wa misaada ya kibinadamu.

Baraza hilo lilipitisha azimio kwenye mkutano maalum wa nane uliomalizika siku hiyo, azimio hilo linafuatilia sana hali mbaya ya haki za binadamu katika sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tokea mwezi Agosti mwaka huu, na kuzitaka pande zote husika zifuate sheria za kimataifa zikiwemo sheria za haki za binadamu na sheria za wakimbizi, na kuwalinda wakazi wa huko.