Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-03 10:51:06    
Washington-Kuimarisha mawasiliano kati ya Marekani na China kunasaidia kukabiliana na msukosuko wa fedha

cri

Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Henry Paulson tarehe 2 alisema kuimarisha mawasiliano kati ya Marekani na China kunasaidia kukabiliana na msukosuko wa fedha kwa hivi sasa , na anatarajia mazungumzo ya tano ya uchumi wa kimkakati kati ya China na Marekani yatakayofanyika hapa Beijing yataendelea kupata mafanikio.

Bw. Paulson siku hiyo alipotoa hotuba kwenye kamati ya mambo ya dunia ya Washington alisema kuwa, China itaendelea kuwa mhusika muhimu kubwa katika uchumi wa dunia, maendeleo ya China ni fursa kwa makampuni na wateja wa Marekani, China yenye utulivu, ustawi na amani inalingana na maslahi ya wananchi wa China, wa Marekani na wa dunia nzima. Marekani na China zimepata mafanikio makubwa katika mazungumzo yaliyofanyika mara nne, na anatarajia mazungumzo ya tano yataendelea kupata mafanikio.