Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-03 14:23:15    
Brussel-Umoja wa Ulaya na Misri zasaini kumbukumbu ya ushirikiano wa nishati

cri
Umoja wa Ulaya na Misri tarehe 2 huko Brussel zilisaini kumbukumbu ya kuzidisha ushirikiano wa pande hizo mbili katika sekta ya nishati.

Kwa mujibu wa waraka huo, Misri itafanya mageuzi ya soko la nishati ili hatimaye kujiunga na soko la nishati la Umoja wa Ulaya, pande hizo mbili zitatafuta nishati endelevu, kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati, kujenga mtandao wa usafirishaji wa nishati, na kushirikiana pamoja katika teknolojia za sekta ya nishati.

Kwenye sherehe ya kusaini kumbukumbu hiyo, Umoja wa Ulaya ulisisitiza umuhimu wa Misri kwa usalama wa nishati ya Umoja wa Ulaya, na Misri ilisema kuwa waraka huo umefungua njia pana kwa ushirikiano wa nishati kati ya pande hizo mbili.