Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-06 18:56:33    
China yapokea michango ya fedha na vitu yenye thamani ya yuan bilioni 75.2 baada ya tetemeko la ardhi

cri

Wizara ya mambo ya raia ya China hivi karibuni ilitoa ripoti ikisema kuwa, baada ya tetemeko kubwa la ardhi kutokea tarehe 12 Mei mkoani Sichuan, watu wa hali mbalimbali nchini China na katika nchi za nje walitoa michango ya fedha na vitu mbalimbali kwa sehemu zilizokumbwa na maafa, michango hiyo inasaidia sana kazi za uokoaji na ukarabati baada ya maafa katika sehemu hizo.

Hadi kufikia tarehe 25 Novemba, China ilikuwa imepokea michango ya fedha na vitu yenye thamani ya yuan bilioni 75.2, kati ya michango hiyo, fedha na vitu yenye thamani ya Yuan bilioni 33.8 imepelekwa kwenye sehemu zilizokumbwa na maafa.