Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-12-06 20:49:15    
Pyongyang-Korea Kaskazini yakataa kuzungumza na Japan kwenye mazungumzo ya pande sita

cri
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Korea Kaskazini tarehe 6 alisema, kwa kuwa mpaka sasa Japan inaendelea kukataa kutekeleza wajibu wake, Korea Kaskazini haitakubali Japan kuwa mjumbe mmojawapo wa mazungumzo ya pande sita, na haitazungumza na Japan tena.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na chombo kimoja cha habari cha taifa cha Korea Kaskazini, msemaji huyo alisema, mkutano wa viongozi wa ujumbe wa mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la Peninsula ya Korea utafanyika hivi karibuni, lengo la mkutano huo ni kuamua mwendo wa pande nyingine tano kuipa fidia Korea Kaskazini kutokana na nchi hiyo imeanza kuondoa uwezo wa zana zake za nyuklia. Mkutano huo pia unatarajiwa kufikia makubaliano katika suala linalohusu ukaguzi wa zana za nyuklia za Korea Kaskazini.