• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Juni-10 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-10 20:37:06

  Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab washambulia makao makuu ya kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia

  Kundi la Al-Shabaab limeshambulia makao makuu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM yaliyoko wilaya ya Halgan, katikati mwa Somalia.

  Mashuhuda wamesema, gari moja lililoendeshwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga lililipuka katika mlango mkuu wa makao makuu hayo yanayotumiwa na vikosi vya Ethiopia vinavyohudumia AMISOM, na kusababisha majibizano ya risasi kati ya pande hizo mbili.

  Kundi la Al-Shabaab limetangaza kuhusika na shambulizi hilo, likisema shambulizi lake limesababisha vifo vya askari 60 wa Ethiopia. Lakini AMISOM imekanusha madai hayo, na kusema vikosi vyake vimewafukuza washambuliaji hao na kuwasaka wapiganaji waliokimbia.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako