• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Juni-10 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-10 20:37:06

  Kampeni ya kura ya maoni yashika kasi Uingereza

  Kampeni ya kura ya maoni ya iwapo Uingereza itajiondoa kwenye umoja wa Ulaya au la imeendelea wiki hii nchini humo.

  Mawaziri wakuu wa zamani nchini Uingereza wamejiunga kwenye kampeni ya kuwashawishi watu nchini humo kutopiga kura ya kuondoka kwenye muungano wa Ulaya.

  Wakiongea huko Ireland Kaskazini, Sir John Major na Tony Blair walisema kuwa kura ya ndio itahujumu mpango wa amani eneo hilo, na kuongeza uwezekano wa Scotland kutaka kuwa huru.

  Sir John alisema wa uamuzi wa kuondoka kwa muungano wa ulaya utakuwa makosa ya kihistoria.

  Kura ya maoni ya kuamua ikiwa Uingereza itaondoka kwenye muungano wa Ulaya au la inafanyika Juni 23.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako