• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Juni-10 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-10 20:37:06

    Upinzani DRC wakubali kushiriki mazungumzo kwa masharti

    Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ettiene Tchisekedi, amesema yuko tayari kwa mazungumzo na rais Joseph Kabila lakini ametoa sharti kuwa mazungumzo hayo yafanyike chini ya usimamizi wa jumuiya ya kimataifa.

    Akizungumza mara baada ya kuhitimisha mkutano wake na wanasiasa wengine wa upinzani aliowaalika mjii Brussels, Ubelgiji, Tshisekedi, amesema walikutana kama wazalendo kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kuhakikisha rais Kabila hawanii urais kwa muhula wa tatu.

    Viongozi hao wamekubaliana kufuata njia za kisheria na amani kuhakikisha Rais Kabila anaondoka madarakani, na wao kujiepusha na vurugu ambazo huenda zikaifanya Serikali kutumia nguvu kuwakabili.

    Mkutano huu umefanyika wakati ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya nje wa Ubelgiji, Didier Raynders akiwa ziarani katika nchi za Maziwa Makuu kujaribu kushawishi kusaidia kupata suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako