• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Juni-10 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-10 20:37:06

  Mashirika mawili ya ndege yafuta safari Nigeria

  Wiki hii mashirika mawili ya kimataifa ya ndege yamefuta safari zao kwenda nchini Nigeria wakati nchi hiyo inapokabiliana na hali mbaya zaidi ya uchumi kwa miongo kadhaa.

  Shirika la ndege la Uhispania, Iberia lilifuta safari zake mwezi uliopita huku shirika la Marekani la United Airlines, nalo likisema kuwa litafuta huduma zake za kila siku mwishoni mwa mwezi Juni.

  Mashirika hayo yanasema kuwa kupungua kwa safari na kudhibitiwa kwa sarafu, ndivyo vyanzo vya uamuzi huo.

  Hii ni ishara ya hali mbaya ya uchumi inayolikumba taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

  Kushuka kwa bei ya mafuta kumesababisha Nigeria kushuhudia ukuaji mdogo na uhaba wa sarafu za kigeni.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako