• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Juni-10 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-10 20:37:06

    Obama amuidhinisha Clinton kuwania urais kwa chama cha democrat

    Wiki hii Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu nchini humo.

    Amechukua hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana na seneta wa Vermont Bernie Sanders ambaye amekuwa akikabiliana na Bi Clinton katika kinyang'anyiro cha kumchagua mgombea wa chama hicho.

    Obama amesema mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa Marekani na kwamba atamuunga mkono kushindana na mgembea wa chama cha Republican Donald Trump.

    Rais Obama pia ametoa wito wa mshikamano ndani ya chama cha Democrat, ili kumzuia Trump kushinda kwenye uchaguzi huo.

    Bernie Sanders naye amesema yuko tayari kufanya kazi na mpinzani wake, Bi Clinton, kumshinda Donald Trump katika uchaguzi mkuu.

    Hata hivyo alisema ataendelea kufanya kampeni yake na kwamba anatumai atakutana na Bi Clinton hivi karibuni.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako