• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Juni-10 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-10 20:37:06

  Takriban watu 30 wauawa Iraq

  Wiki hii wapiganani wa kundi la IS wameendesha mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga ndani na nje ya mji wa Iraq, Baghdad ambapo takriban watu 30 wameuawa.

  Shambulizi la kwanza lilikuwa la gari ambalo lililipuka eneo lenye washia wengi ndani ya mji wa Baghdad ambapo watu 19 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

  Shambulizi la pili lililenga kizuizi cha wanajeshi kaskazini mwa Baghdad ambapo watu 11 waliuawa wakiwemo wanajeshi.

  Islamic state imejikita katika mashambulizi ya mabomu mjini Baghdad hivi majuzi wakati jeshi la Iraq, linaendelea na oparesheni kubwa kulitimua kundi hilo kutoka ngome yao ya mji wa Fallujah, kilomita 60 magharibi mwa Baghdad.


  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako