• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Juni-17 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-17 18:47:34
  Polisi wakamata waasi 26 kusini mwa Burundi

  Wiki hii waasi 26 wamekamatwa na kunyang'anywa silaha zao na polisi kwenye sehemu ya kusini mwa Burundi baada ya siku ya mwisho iliyotolewa na rais Pierre Nkurunziza kujisalimsha kupita.

  Msemaji wa polisi wa Burundi Bw. Pierre Nkurikiye amesema kutokana na kumalizika kwa muda wa siku 15 uliotolewa na rais Nkurunziza kwa waasi kujisalimisha, waasi 26 walikamatwa kwenye maeneo manne.

  Waasi wanne walijisalimisha na silaha zao kwa jeshi la usalama. Amesema polisi pia walikamata bunduki sita na guruneti moja.

  Mwanzoni mwa mwezi huu wa Juni Rais Pierre Nkurunziza alipofanya ziara kusini mwa Burundi alitoa siku 15 kwa makundi yenye silaha kujisalimisha kwa vikosi vya serikali.

  1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako