• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Juni-17 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-17 18:47:34

    CIA yaonya kuhusu mashambulizi zaidi kutoka kwa kundi la IS,

    Baada ya watu 49 kuuwawa na mtu aliyedai kuwa mfuasi wa kundi la IS wiki hii nchini Marekani, mkurugenzi wa Shirika la upelelezi nchini humo CIA Bw John Brennan amesema kundi la IS nchini Syria na Iraq linajaribu kutuma wapiganaji wake kufanya mashambulizi zaidi kwenye nchi za magharibi.

    Hata hivyoLakini amethibitisha kuwa muuaji wa Orlando hakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kundi la IS.

    Bw Brennan amesema kundi la IS lina wapiganaji wengi kutoka nchi za magharibi ambao wanaweza kutumika kufanya mashambulizi katika nchi za magharibi, ameonya kuhusu uwezekano wa kundi hilo kujipenyeza kwenye kambi za wakimbizi. 

    Bw Brennan amesema licha ya juhudi kubwa zilizofanywa, juhudi hizo hazijaweza kukomesha uwezo wa kundi la IS kufanya mashambulizi katika sehemu mbalimbali dunia. Licha ya kutwaa eneo kubwa kutoka kwa kundi hilo, kundi hilo bado lina wapiganaji kati ya elfu 18 na elfu 22, na tawi lake la Libya ni tawi kubwa zaidi.

    Amesema changamoto kubwa zaidi kwa wana intelijensia kwa sasa ni washambuliaji wa kujitegemea.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako