• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Juni-17 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-17 18:47:34

    Umoja wa Mataifa wakubali kambi ya wakimbizi ya Daadab, ifungwe

    Hatimaye Umoja wa Mataifa wiki hii umeunga mkono juhudi za Kenya za kuwarudisha maelfu ya wakimbizi raia wa Somalia nchini mwao na kuifunga kambi ya wakimbi ya Dadaab ifikapo mwezi November mwaka huu.

    Uamuzi huu umekuja baada ya rais Uhuru Kenyatta kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, jinini Brussels nchini Ubelgiji.

    Kenya imekuwa ikisema itawarudisha nyumbani wakimbizi hao na kuhakikisha kuwa wanaondoka kwa usalama, ikisema sababu yake kuu ni ya kiusalama.

    Moon amesema, Umoja wa Mataifa utatafuta fedha ili kuisaidia Kenya kuwarudisha nyumbani wakimbizi hao kwa njia nzuri na ya kibinadamu.

    Hatua za mwisho yza kuwaondoa wakimbizi hao nchini Kenya, zitajadiliwa mwezi ujao pembeni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na maendeleo utakaofanyika jijini Nairobi mwezi ujao.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako