• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Juni-17 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-17 18:47:34

    Jeshi la Nigeria lawaokoa mateka 57 kutoka kundi la Boko Haram

    Msemaji wa jeshi la Nigeria Kaneli Sani Usman jana amesema, vikosi vya doria vimewaokoa mateka 57 kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram kwenye majimbo ya kaskazini ya Adamawa na Borno.

    Bw. Usman amesema, mateka hao wakiwemo wanawake na watoto wamepelekwa kwenye vituo vya kijeshi vya karibu, ambapo watapata huduma za upimaji afya na matibabu.

    Bw. Usman amesema askari wa Brigade Garrison ya 22 wamewaokoa mateka 14 kutoka kwa kundi la Boko Haram wakati walipofanya doria kwenye kijiji cha Chingowa karibu na sehemu ya Dikwa. Na kikosi maalumu cha 114 kinachofanya doria kwenye barabara kati ya Izge na Bitta kimewaokoa mateka 43 huko Madube.

    Msemaji huyo pia amesema wapiganaji wawili wa Boko Haram wameuawa, huku askari watatu wa jeshi la Nigeria na raia 13 wakijeruhiwa kwenye mashambulizi wakati wa kufanya doria karibu na Gwoza.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako