• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Juni-17 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-17 18:47:34

    Rais wa Afrika Kusini asema kuna matumaini kwenye eneo la maziwa makuu

    Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema wiki hii kwamba kuna matumaini kuwa masuala magumu ya migogoro na kukosekana kwa utulivu katika eneo la maziwa makuu yatatatuliwa.

    Rais Zuma amesema hayo baada ya mkutano wa 6 wa kimataifa wa viongozi wa eneo la maziwa makuu uliofanyika mjini Luanda, Angola Amesema ripoti kamili kuhusu mkutano huo itawasilishwa kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Afrika nchini Rwanda.

    Mkutano huo ulijadili hali ya kisiasa na usalama kwenye nchi za eneo la maziwa makuu zikiwemo Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya demokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

    Mkutano huo pia umechagua katibu mkuu mpya, na kuthibitisha Angola kuwa mwenyekiti wa kundi hilo kwenye muhula mwingine.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako