• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (11 Juni-17 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-17 18:47:34

    Wasomali 18 wafa ndani ya bohari nchini DRC kwa kukosa hewa

    Polisi nchini Zambia, wanasema wiki hii kuwa wahamiaji 18 wenye asili ya Kisomali, wamefariki walipokuwa wakipelekwa kwa njia haramu kuingia katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

    Walikuwa wamebebwa ndani ya bohari lililokuwa na mzigo wa Samaki lakini wakafariki kutokana na kukosa hewa.

    Kamishina mmoja mkuu wa polisi nchini Zambia Hudson Namachila, amesema kuwa lori hilo lilisimama ndani ya mpaka wa Kongo pale baadhi ya wahamiaji haramu waliokuwa wameishiwa na hewa, walipoanza kugonga gonga bohari hilo wakiwa ndani, kuwaashiria madereva wawafungulie ambao walikuwa wamekamatwa.

    11 kati ya wasomali hao 44 tayari walipatikana kuwa wamekufa huku wengine saba wakifariki baadaye na 27 walionusurika kufa wametiwa mbaroni.

    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako