• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Juni-24 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-24 18:30:33

    Uingereza yajitoa kwenye Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni ya kihistoria

    Wiki hii raia nchini Uingereza wamepiga kura kuunga mkono nchi hiyo kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Tume ya Uchaguzi ya Uingereza imesema, nchi hiyo imejitoa kwenye Umoja huo kutokana na asilimia 51.9 ya kura kuunga mkono hatua hiyo.

    Msimamizi wa hesabu za kura ya maoni kuhusu Umoja wa Ulaya Jenny Watson ametangaza kuwa, Waingereza milioni 17.4 wamepiga kura ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya dhidi ya milioni 16.1 waliotaka nchi hiyo kuendelea kuwa mwanachama wa Umoja huo.

    Lakini vyombo vya habari vya Uingereza vinaripoti kuwa, mchakato wa kujitoa kwenye Umoja huo hautaanza mara moja na utachukua muda mrefu.

    Wakati huohuo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ametangaza nia yake ya kujiuzulu mara baada ya nchi yake kupiga kura ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako