• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Juni-24 Juni)

    (GMT+08:00) 2016-06-24 18:30:33

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa vikwazo dhidi ya makundi ya wapiganaji ya DRC

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitia azimio la kuongeza muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya makundi mbalimbali ya watu wenye silaha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hadi tarehe mosi, Julai, mwakani.

    Azimio hilo limesema makundi hayo yanaendelea na shughuli za kijeshi, biashara magendo ya dhahabu na pembe za ndovu na kusababisha tishio la usalama na mgogoro wa ubinadamu.

    Kwa mujibu wa azimio hilo, nchi zote hazipaswi kutoa misaada na mafunzo ya kijeshi kwa makundi hayo. Pia zinatakiwa kuendelea kupiga marufuku kusafiri na kuzuia mali za wale walioharibu amani na utulivu wa DRC.

    Na huko huko DRC wiki hii Mamlaka, zinawashikilia watu zaidi ya 75 kwa tuhuma kuwa ni wapiganaji wanaosakwa kwa vitendo vya mauaji na ubakaji, kwenye jimbo la Kivu Kusini.

    Mtandao wa kundi hili la wapiganaji, unatuhumiwa kuwalenga wasichana wadogo, wanaowahusisha na imani za kishirikina kuwa wanawapa ulinzi.

    Miongoni mwa watu wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama, ni pamoja na anayetuhumiwa kuwa ni kiongozi wao, Frederic Batumike, ambaye ni naibu gavana.

    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako