• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Juni-24 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-24 18:30:33

  Obama aongea na Kenyatta kuhusu wakimbizi

  Rais wa Marekani Barrack Obama wiki hii amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Kenya Kenya Uhuru Kenyatta kuhusu kufungwa kwa kambi ya wakimbizi ya Daadab inayowapa hifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia.

  Obama amemwambia Kenyatta umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kuwasadia wakimbizi wanaoishi katika nchi hiyo.

  Ripoti zinasema kuwa viongozi hao wamekubaliana kushirikiana kwa mataifa yao, kuhakikisha kuwa haki za wakimbizi hao zinalindwa na kuheshimiwa.

  Kenya imepanga kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Somalia, kufikia mwisho wa mwaka huu.

  Nairobi inasema, sababu kubwa inayowasuma kufikia uamuzi huo ni ya kiusalama baada ya kubainika kuwa, kambi hiyo imekuwa ikitumiwa na wanamgambo ya Al Shabab kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

  Wiki iliyopita, rais Kenyatta alikuwa ziarani jijini Brussels nchini Ublegiji na kukutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na kujadiliana kwa kina kuhusu hatima ya wakimbizi hao.

  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako