• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (18 Juni-24 Juni)

  (GMT+08:00) 2016-06-24 18:30:33

  Burundi yachukua hatua kupambana na homa ya manjano

  Serikali ya Burundi imetangaza kuchukua hatua za kuzuia ugonjwa wa homa ya manjano kuingia nchini humo kutokana na ripoti kuwa ugonjwa huo upo kwenye nchi za jirani.

  Msemaji wa wizara ya afya na kupambana na UKWIMI Thadee Ndikumana amesema wamechukua hatua hizo baada ya kupata ripoti kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Angola, Tanzania na Uganda.

  Bw Ndikumana amesema wameyaagiza mashirika ya usafiri kuwa yanatakiwa kuhakikisha kuwa wasafiri wana vyeti vya homa ya manjano kabla ya kuwapatia tiketi, na wale watakaoingia Burundi bila vyeti hivyo watarudishwa walikotoka.

  Warundi na wageni wanaoishi Burundi pia wametakiwa kufuata kanuni ya kupata chanjo siku kumi kabla ya kusafiri.

  1 2 3 4 5 6 7
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako